Karibu msomaji wa
edonetz katika makala ya kila siku na leo tuangazie katika suala la
ndoa Matarajio ya wanandoa hasa wanawake katika ndoa zao huwa ni mali, starehe
za kupindukia na mengine mengi kama alivyokuwa anayaona katika enzi za uchumba,
lakini kwa bahati mbaya kuwa kwenye ndoa hakuna sehemu ya kuweka wazi maslahi
binafsi basi husubiri kuona kama miujiza itatokea.
Lakini kwa walio wengi
hujisahau jambo ambalo huifanya ndoa kuwa chungu na hatimaye kufarakana wakati
ndoa ikiwa mbichi. Hila unahitajika umakini katika vitu vifuatavyo.
UPENDO
Upendo wa kweli ni jambo muhimu katika maisha
ya ndoa, vijana wengi hukimbilia ndoa kisa mali hasa vijana wa kike, bila
kusahau ndoa ni pingu za maisha na huyo mtu utakaa naye milele. Upendo wa kweli
usipokuwepo katika ndoa haiita dumu kwani amani haitakuwepo, pia faraja
kati ka wanandoa haitopatikana na ndoa hiyo hugeuka maigizo.
UVUMILIVU
Ndoa imeundwa na watu
wawili ambao walitoka nyumba tofauti, malezi na maisha tofauti, ndoa
huwajumlisha kutokana na tofauti zao, kabla ya ndoa kuna kitu kinachoitwa
courtship (Uchumba) hiki ni kipindi ambacho wapenzi hujuliana tabia zao na
kuunganisha tofauti zao na kawaida hutumia mwaka 1 mpaka 4 na ikizidi hapo ni
tatizo, kukiruka au kukizidisha kipindi hiki huharibu ndoa nyingi na kama
hapakuwa na maelewano ya tabia hapa mnaruhusiwa kuachana na kama ukilazimisa
ndoa hiyo haitadumu.
UAMINIFU
Kama upendo wa kweli
ukiwepo ndani ya nyumba, uaminifu hasa ndio huhitajika, kama hamta aminiana
vitu vidogo vitawatenganisha, maana jamii kawaida huonea wivu ndoa na kutupa
mishale ya maneno na matendo ili kuijeruhi ndoa, siri za ndani zinapaswa
kuishia baina ya wanandoa, na kama uaminifu hauta kuwepo ndoa itakuwa
mashakani na nivigumu kudumu.
MSAMAHA
Kuna msemo wa Kiswahili
unasema “hakuna aliye mkamilifu” hii
inamaanisha kwamba binadamu hukosea na anahitajika kusamehewa, kama ndoa haita
weka msamaha kama ngao yao, mhimili wa ndoa hii upo matatani.
MAWAZO MGANDO
Katika ndoa wanawake
wengi huwategemea wanaume katika kutafuta na hata wengine wakijiita ni wanawake
wa nyumbani, pia kuna wanaume wanaolelewa, ndoa haiwezi kuendelea kama
hapatakuwa na maendeleo maana mtapata watoto na kipato toka uchumba hadi watoto
watatu hali ni ile ile mwisho wa siku ndoa huvunjika kisa kipato shida.
Mwanandoa kutumia njia
mbadala (wizi, uzinzi n.k), kwa mwanamke epuka kuwa mke wa nyumbani na
mwanaume atafute kazi, hii pia husaidia katika tendo maana wote mnakuwa
mmechoka tendo mnafanya kutafuta usingizi, vinginevyo ndio mchepuko unapoanzia.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv