MAHITAJI
Yai,asali,sukari laini ya unga,limao,manjano,nyanya iliyoiva vizuri lakini ngumu,bakuli mbili,liwa,sabuni,taulo laini na safi na moisturizer.

JINSI YA KUFANYA
Safisha vizuri uso kisha kausha kwa taulo,usiache maji yakaukie yenyewe usoni,sio vizuri.
Chukua nyanya uliyoisafisha vizuri kisha ikate katikati kisha inyunyuzie sukari,halafu sugua nayo usoni taratibu sana bila kujichubua ,sugua kama unachora maduara kuanzia kidevuni kwenda kwenye paji la uso,usianzie juu kwenda chini siku zote anzia chini kwenda juu.

Kitendo hiki /exfoliation husaidia kuondoa ngozi zilizokufa,kufungua vitobo katika ngozi,hivyo ngozi kupumua vizuri maana ngozi isipoingiza hewa mtu anaweza kupata chunusi.Ukishafanya hivyo kwa kama dk 2 then acha ibakie hivi hivi usoni then;

Chukua yai lipasue katikati ukihakikisha kuwa kiini hakivurugiki,kishatenganisha ute mweupe kwenye bakuli lake na kiini kwenye bakuli lake,Kisha chukua bakuli lenye kiini weka manjano,asali,matone ya limao na liwa kisha koroga upate mchanganyiko unaoona utanata usoni bila kuchuruzika.Kila kitu pima kulingana na jinsi wewe unavyoona itatosha kukupatia mchanganyiko usio mwingi wala kidogo sana na wala usio mgumu wala mwembamba sana.Then;

Safisha uso kuondoa zile nyanya na sukari,jikaushe then jipake huu mchanganyiko ukae nao kwa dk 10-15 au zaidi kama muda unaruhusu.

Baada ya hapo,safisha vizuri uso wako huku ukisugua sugua kama kuna ngozi zilizokufa zilizobakia zitoke zote kisha jikaushe halafu;

Chukua lile bakuli lenye ute mweupe wa yai,(hakikisha kiini hakijaingia humu hata kidogo),chukua uma kisha pigapiga huo ute hadi uwe kama povu halafu jipake usoni kwa wingi mara moja kisha toka nje upigwe na upepo ambao utasaidia kukausha kwa haraka huo ute.Kadiri ute utakavyokua ukikauka usoni mwako utaona kuwa ngozi ya uso wako inajivuta na kuwa tight.Kaa na huu ute kwa dk 10-15 kama unaweza kukaa nao zaidi ni vizuri.Hii inasaidia kukaza misuli ya uso hivyo kuzuia wrinkles au kama zipo inasaidia kuziondoa maana wrinkles huja pindi misuli ya uso inapokua imelegea.

Baada ya hapo safisha uso paka moisturizer/lotion yako.

Ukifanya hivi kila wiki mara moja baada ya mwezi utaona jinsi ngozi yako inavyobadilika,ila hata siku ya kwanza utaona ngozi yako haiko kama ilivyokua kabla ya kufanyahivi.

kumbuka
Vipo vitu vingi sana vya asili vinavyotumika na sio mbaya kuongeza vitu vingine kama kitunguu saumu,matango,wengine maziwa,unga wa dengu na vingine vingi ila kuna watu wanachanganya pia na mafuta ya mawese,kabla ya kuchanganya mawese kwenye mchanganyiko wako ni lazima uwe na uhakika wa asili mia moja kuwa ngozi yako haitareact vibaya baada ya kujipaka haya mafuta.Kuna ngozi hazitaki mafuta,hivyo mtu unaweza kujipaka mawese ukashangaa umepata chunusi za kufa mtu.
Bottom of Form

  
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top