Siku hizi mambo
yamebadilika sana. Ukitokea kumpenda mtu fulani kama kweli nia yako ni
kuingia naye kwenye ndoa na siyo kukidhi matamanio ya siku moja, zipo
mbinu nyingi zinazoweza kukurahishia kazi yako. Kuna simu za mikononi,
kuna mitandao ya kijamii na njia chungu nzima hivyo huna haja ya kuendelea
kuumia na upweke.
Na lazima ujue kuwa
penzi bora ni lile ambalo wawili huanza kwa kuwa marafiki, ni makosa
kukurupuka kumtongoza mtu kwenye simu au kwenyemitandao ya kijamii bila kumvuta
kwanza karibu yako na kumfanya kuwa rafiki yako.
Unatakiwa kujitahidi kujenga ukaribu naye,
Kama unadhani ni vigumu
kwa wewe na yeye kukutana ana kwa ana, unaweza kutafuta namba yake ya
simu. Ukishapata namba ya simu ya huyo umpendaye, tafuta muda ambao
utakuwa umetulia kisha mpigie na jitambulishe.
Mweleze kwamba umempigia simu kumjulia hali,
Kama akikuuliza
mahali ulikoipata namba yake, unaweza kumjibu vyovyote lakini
inashauriwa kuwa siyo vizuri kumtajia aliyekupa namba yake kwa sababu
unaweza kuwagombanisha.
Usiwe na papara,
Mtakie siku njema na
endelea na shughuli zako nyingine. Unaweza pia kuendelea kumtumia meseji
za kawaida (siyo za mapenzi), ukimjulia hali, ukimuuliza kama
ameshakula au amekula chakula gani, anafanya nini kwa muda huo na vitu
anavyovipenda sambamba na vile asivyovipenda.
Tumia sauti ya utulivu yenye hisia ndani yake,
Utazidi kumvuta
karibu yako, Usipende kuzungumza kwa sauti ya juu au kupayuka au kupiga
simu ukiwa kwenye kelele, akipokea tu simu yako, mjulie hali yake
kisha msifie kidogo kuhusu sauti yake na namna anavyozungumza.
Badili mazungumzo,
Muulize kama anajua
kwamba yeye ni mzuri sana na hujawahi kukutana na mtu anayevutia kama
yeye. Kama wewe ni mwanaume na unayezungumza naye ni mwanamke, utakuwa
katika nafasi nzuri ya ‘kum-win’ kwa sababu wanawake wengi wanapenda sana
kusifiwa.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv