Tatizo la ukosefu wa
ajira ni suala ambalo limeendelea kuwatesa vijana wengi wa Kitanzania, licha ya
takwimu za uchumi kwa mwaka jana kuonesha kukua kwa wastani wa asilimia 7.1 na
kufanya vizuri katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ingawa umasikini
haujapungua kama ilivyotegemewa na Watanzania.
Lazima ujue kuwa sio
kweli kwamba mtaji pekee ndio kikwazo, lakini wengi wanaamini mtaji ndio
unawazuia. Lakini pia wakati huo ambao mtu hana mtaji hakuna juhudi anazofanya
kuhakikisha anapata mtaji huo.
Sasa JIONGEZE na
biashara hizi tano unazoweza kuanza kuzifanya bila ya kuanza na mtaji wa fedha.
Biashara ya uwakala wa
mauzo (salesman)
Kuna makampuni
mbalimbali ambayo yanatumia mawakala kuuza bidhaa au huduma zao. Kwa wewe
kujifunza na kuwa wakala wao unaweza kupata kipato kizuri kwa njia ya
kamisheni.
Biashara ya mtandao
(Network marketing)
Hii ni biashara ambayo
ni mkombozi kwa mtu yeyote ambaye ana kiu ya kufikia mafanikio. Hapa Tanzania
kuna makampuni mengi yanayofanya biashara hii kama Forever Living, Oriflame,
GNLD, na mengineyo. Katika makampuni haya kuna ambayo unaweza kuanza na kiasi
kidogo cha fedha ambacho ni sawa na bure.
Biashara ya ushauri
Je kuna kitu ambacho
una utaalamu nacho? Je kuna kitu ambacho unapenda kukifuatilia na hivyo
unakijua sana? Vizuri, kuna mtu anataka kukijua ila hajui aanzie wapi.
Kama wewe mmoja wa wanaoweza kutoa ujuzi na uzoefu kwa wengine
unaweza kulipwa fedha.
Biashara ya taarifa
(internet marketing)
Hii ni biashara ya
kutoa taarifa kwa kupitia mtandao wa intaneti. Unaweza kuwa na ‘blog’
ambayo ni bure kuiendesha na baadaye ukaanza kupata kipato kizuri kupitia
matangazo.
Biashara ya udalali
Hii ni biashara ambayo
wewe unamsaidia mtu kupata kitu anachotaka na hana muda au uzoefu wa kukipata.
Kama ukiweza kuifanya biashara hii kwa mbinu nzuri unaweza kutengeneza kipato
kizuri.
Kumbuka; Biashara hizi zinahitaji ubunifu na kujituma
tena kwa bidii na maarifa ingawa unaweza usione faida au mafanikio mapema. Ila
ukiweka malengo na mipango mizuri utaona mafanikio makubwa baadaye. Uzuri
ni kwamba unaweza kuanza biashara hizi ukiwa bado umeajiriwa au upo masomoni.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv