Eyeshadows ni urembo ambao hutumiwa juu na chini ya kope.
Njia hii husaidia kuongeza kina na mwelekeo wa macho ya watu. Watu wanapenda
kutumia aina hii ya urembo ili kuweza kuimarisha muonekano wao.
Kama wewe ni mweusi jaribu kutumia rangi angavu ili kuimarisha muonekano wako ukitumia rangi za giza zitakufanya uonekane vibaya.
Ni muhimu kuhakikisha kuwa unakuwa makini ili kuweza kuweka macho yako katika hali bora zaidi ya kupendeza.
Wakati mwingine Eyeshadows hufanya macho kuonekana makubwa au madogo. Lakini cha muhimu kuzingatia je rangi unayopaka inaendana na macho yako au ngozi yako.
Unatakiwa kupaka rangi
kwa ustadi mkubwa huku ukiweka mkolozo katika kona za macho yako.
Ni vizuri kama utatumia eyeshadow ya penseli kwani huwa rahisi kuitumia na inapatikana kwa urahisi madukani.Kuna rangi za aina nyingi ambazo hupendeza wapakaji, rangi hizo ni pamoja na pink plum, matumbawe na shaba, bluu na kijani pamoja na fedha, dhahabu na nyingine nyingi.
Rangi hizi hutofautiana kulingana na mng'ao wake kwani kuwa zenye mng'ao mkubwa na zile zilizofifia.Njia ya kawaida ya kupaka eyeshadow ni kutoka ndani ya kona ya jicho na nje na zaidi.
Rangi kama Gray, violet, zambarau na bluu huwapendeza sana watu wa rangi ya maji ya kunde
na kusaidia kung'arisha macho yao.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv