Bamia ni mboga ambayo inafahamika na watu wengi hasa watanzania na imekuwa ikitumiwa na watu wengi hapa nchini.

Pamoja na kuwa mboga hii kuonekana ni ya watu wenye kipato cha chini, lakini pia ina faida nyingi katika miili yetu.

Bamia husaidia kuondoa uchovu wa mwili pamoja na kusaidia kutibu tatizo la kukosa choo.
 

Aidha, bamia pia inaelezwa kusaidia kusafisha damu, kutibu mafua, vidonda vya tumbo, inaimarisha mifupa pamoja na kuwa kinga ya magonjwa kama utapiamlo na anemia.

Mboga hii imekuwa ni msaada kwa watu wenye matatizo ya mifupa au maumivu ya viungo kwani huongeza uteute kwenye viungo vya mifupa, ili upate faida hii inakupasa ule bamia kama supu.
 
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top