Kama ambavyo nadharia mbalimbali zimeeleza juu ya
uumbaji wa binadamukwamba kaumbwa na mungu wengine katokana na sokwe. Sasa vivyo hivyo kwa upande wa mwezi
zipo nadharia kadha wa kadha zinazoelezea uwepo wake. Katika miaka mingi
iliyopita wanajimu hawakupata maoni ya pamoja kuhusu jinsi mwezi ulivyozaliwa.
Kimsingi waliwahi kutoa nadharia nne kuhusu chanzo cha mwezi.
NADHARIA YA KWANZA ni kwamba mwezi uligawanyika
kutoka katika dunia yetu. Mwaka 1898, mnajimu george howard darwin alisema
mwanzoni mwezi ulikuwa ni sehemu moja ya dunia, lakini dunia ilizunguka kwa
kasi kupita kiasi na kusababisha mwezi kugawanyika katika dunia. Lakini sampuli
za miamba ya mwezi zilizopelekwa duniani na chombo cha anga ya juu zinaonesha
kuwa miamba ya mwezi ni tofauti kabisa na ile ya dunia, hivyo nadharia hii si
sahihi.
NADHARIA YA PILI ni kwamba mwezi ni kimondo
kilichovutwa na dunia. Baadhi ya wanajimu wamekanusha nadharia hii, kwani mwezi
si mdogo, dunia haina mvuto mkubwa wa kutosha kuvuta kimondo kikubwa kama hiki.
NADHARIA YA TATU inasema hewa na vumbi kwenye
mfumo wa jua vilikusanyika pamoja na kuunda mwezi na dunia, hivyo vina chanzo
cha pamoja. Lakini nadharia hii pia imekanushwa, kwa sababu sampuli za miamba
ya mwezi zinaonesha kwamba mwezi una historia ndefu zaidi kuliko dunia.
NADHARIA YA NNE imekubaliwa na watu wengi zaidi, inasema wakati dunia ilipoanza kuundwa,
iligongwa na kimondo. Vipande vya kimondo hiki vilikimbilia duniani, lakini
kutokana na mvuto wa dunia, havikwenda mbali na kukusanyika pamoja na kuunda
mwezi.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv