Mahojiano haya maarufu kwa
jina la usaili wa ajira, yanaweza kufanywa kwa mazungumzo ya ana kwa ana au
hata kwa maandishi kupitia taratibu kama mitihani.
Kwa kawaida, usaili
unafanywa kama njia muhimu ya mwajiri kung’amua sifa za mtu anayetaka kumpa
majukumu ya kikazi.
Ili ushinde usaili kuna
mbinu unazoweza kutumia kuwashawishi watu wanaokuhoji, wakupe wewe majukumu
hayo na siyo wengine ambao ni washindani wako.
Kwa mujibu wa kitabu
kiitwacho UK’s Leading Interview
Expert , UTULIVU ni moja ya silaha kubwa
anazotakiwa kuwa nazo muomba ajira anapokuwa mbele ya jopo la watu wanaomuuliza
maswali.
Maelezo
yanasema; Unapoingia
kwenye chumba cha usaili, jenga utulivu wa akili, mwili kwa kufuata maelekezo
kutoka kwa wanaokufanyia usaili. Jenga uso wa tabasamu huku ukijiweka tayari
kujibu swali kwa ufasaha na kuzingatia mipaka ya swali lako.
Kitabu
kinaongeza kusema: Wazoee
kwa haraka watu wanaokusaili kuwa sehemu yao na wao wawe sehemu yako. Hili
utalifanya kwa kuondoa hofu. Wachukulie kama rafiki zako wa karibu ambao
mnaweza kuzungumza na kujadili jambo lolote kwa uhuru.
Mdau wa masuala ya ajira, Cheryle Palmer anasema UKWELI ni jambo la muhimu, siku
zote sema ukweli katika usaili kwa kuwa utakusaidia kukuongoza.
Epuka kuweka maelezo kwa
lengo la kupata sifa zinazoweza kukugharimu itakapobainika kwamba kuna taarifa
hazioani na siyo za kweli,
USIFANYE MAKOSA HAYA KWENYE USAILI
Mwandishi Susan Joyce wa Uingereza anayataja makosa 10 ambayo
unapaswa kuyaepuka unapokuwa kwenye usaili.
1.Epuka
kuvaa mavazi yasiyo na staha au muonekano usio na staha wala
unadhifu.
Kumbuka kwamba usaili huhusisha watu wengi. Katika usaili epuka mavazi
yasiyoruhusika katika maadili au sehemu za kazi..
2.Jiandae, usipojiandaa kwa ajili ya usaili unaweza kupoteza ya
nafasi kuchaguliwa. Kutojiandaa kutakufanya kujibu maswali kinyume na matarajio
ya unachooulizwa.
3.Epuka
hasira.
Usithubutu kuingia chumba cha usaili ukiwa na hasira. Wakati mwingine unaweza
kuulizwa maswali ya uchokozi. Dhibiti hisia zako na jibu maswali husika bila
kukasirika.
4.Epuka
kutoa maelezo mengi yasiyohitajika. Kueleza mambo mengi, kunaweza kukutoa nje ya
mada.
5.
Kuwa makini na matumizi ya lugha za mwili au ishara. Kwa mfano, unapojibu kwa
kutumia kichwa au kutoa miguno, hautawezesha wanaokuhoji kupata kile
walichotarajia.
6.
Ukipewa nafasi ya kuuliza maswali, usiulize mambo yasiyohusiana na ajira
unayoomba.
Aidha epuka maswali yanayoweza kuwapa wasiwasi waajiri wako.
Swali kama je, mkiniajiri
mtanipatia usafiri, ni aina ya maswali yanayoweza kumpa mwajiri wako nafasi ya
kubaini udhaifu wako tangu mapema. Unaweza kuuliza swali kama; nini siri ya
wateja wenu kusifu huduma mnazotoa?
Swali hili linakujenga kwa
kuwa mwajiri anaweza kukutazama kama mtu unayefuatilia kwa karibu masuala ya
ofisi yake. Pia swali hili ni ishara kuwa umefanya utafiti kuhusu ofisi husika.
Aidha, unaweza kuuliza
matarajio yako kuhusu usaili huo kwa kuuliza swali kama, lini nitarajie majibu
ya usaili?
7.
Epuka matumizi ya simu ukiwa kwenye usaili.
8.
Achana na majibu mafupi hasa ya ndiyo na hapana. Ukilazimika kujibu hivyo,
hakikisha unatoa na mifano kadhaa ili kufanya jibu lako liwe na mawanda mapana
zaidi.
9.
Jibu maswali ukilenga maeneo ambayo unayafahamu vyema. Jibu swali ukioanisha na uzoefu ulionao kwa kufanya kazi
katika ofisi ulizowahi kufanya kazi kabla.
10.
Usionyeshe udhaifu wako. Jikite katika kuelezea mafanikio hasa kama umewahi
kufanya kazi maeneo mengine. Kama ni mhitimu, mwelekeo uwe ni kuonyesha namna
utakavyotekeleza majukumu yako kwa ufanisi, hasa ukioanisha elimu uliyonayo na
majukumu unayaomba.
Ukilazmika kuelezea kuhusu
udhaifu wako, tumia udhaifu huo kama nguvu ya kukujenga. Kwa mfano, unaweza
kutaja udhaifu wa kuwa na pupa ya kufanya kazi, ukijenga hoja kuwa hali hiyo
inakuwezesha kupenda kufanya kila kazi kwa haraka na kwa muda.
JIUNGE
NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv