Tatizo  hili la madoa sugu, kwenye maisha ya kawaida ambalo limekuwa likiwasumbua wengi hasa pale unapovaa nguo na zinapoingia madoa, inaweza ikawa umehangaika na kufikia hatua ya kutupa nguo kwa ajili ya madoa sugu na kuhangaika na madawa ya kutoa madoa na kutumia sabuni mbalimbali bila mafanikio.
Njia zifuatazo zitakusaidia kuondoa madoa sugu na kufurahia kuvaa nguo yako
Maziwa; Unaweza kushangaa lakini hii ni dawa nzuri ya kuondoa madoa sugu, kivipi unaweza  kuloweka nguo yako ndani ya maji na kutoa na kuimwagia maziwa halafu ukaiacha kwa muda wa saa kadhaa na utakapoifua utaikuta nguo yako au ya mtoto ipo na hali nzuri bila madoa.

Shampoo; hii ni sabuni ya kuoshea nywele lakini  imeigundulika ina uwezo wa kuondoa madoa hata yalio sugu na kuna madoa yale sugu yanayopatikana kwenye kola za mashati kwa hivyo inasaidia kutoa kwa haraka sana kuliko kupoteza hela kutumia madawa ya kuondoa madoa.

Sprei za nywele; hii inatumika kuondoa madoa yanayosababishwa na peni, ipulizie sprei ya nywele kwenye nguo yenye madoa ya nyewele ili kuweza kuondoa madoa hayo mara moja.

Dawa ya Meno; licha ya kuwa na kazi ya kusafisha kinywa, lakini dawa ya meno pia ni kiboko kuondoa madoa sugu lakini inapaswa kujua kuwa sio kila doa linaweza kutolewa na dawa hii ya meno.

Mkate; licha ya kuwa ni kitafunwa hasa kwa nyakati za asubuhi, lakini mkate unaondoa madoa ya lipstiki ambayo imeingia kwenye nguo kwa urahisi.

Soda; soda hasa Cola inasaidia  kuondoa madoa ya damu kwenye nguo yako sasa hapo inabidi uiloweka usiku na asubuhi uifue itakuwa imetoka madoa. 
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top