Kwa wenye ngozi kavu inahitaji kuimantain ili kuhakikisha inakuwa ngozi ya kawaida kabisa kwani ukiiacha amini kuwa ndio unaiharibu kabisa. Unaweza kuwa una ngozi nyororooo na ukasahau kabisa kuwa uliwahi kuwa na ngozi kavu kwa kufuata yafuatayo.
Tumia maji ya vuguvugu masafi na si ya moto
Maji ya moto husababisha ngozi kuwa kavu zaidi, unachotakiwa ni kutumia maji ya vuguvugu ambayo ni masafi .
Paka mafuta ya kulainisha mikono kila unaponawa mikono.
Kama unahisi mikono yako inakakamaa na inakuwa migumu kila unaponawa hakikisha unapaka mafuta ya kulainisha mikono kama ‘moisturizers’, hii inamaana kuwa ngozi yako inakiu sana ya mafuta unachotakiwa ni kuhakikisha unapaka mafuta ya kutosha.
Paka mafuta ya nazi
Ngozi yako ikiwa kavu paka mafuta ya nazi ambayo ni asilia kabisa au mafuta ya almond, baada ya hapo paka cream hii itakusaidia kwa kiasi kikubwa kulainisha ngozi yako .Watu wengi hupaka mafuta kwenye mwili kama kawaida lakini huwa hawapaki mafuta ya kulainisha hivyo unachotakiwa ni kufuata hatua zote achana na ile hali ya kawaida kwamba ukishapaka mafuta tu basi unatakiwa kupaka na mengine ya kulainisha.
Fanya scrub mara mbili kwa wiki
Ili kuwa na ngozi laini ambayo haiwezi kupauka na kushauri kuifanyia scrub mara mbili kwa wiki, cha muhimu ni kutafuta Scrub nzuri au ya asili ambayo ninao uhakika kuwa itakusaidia kama utaitumia na kufuata maelekezo.
Unaweza kutumia mafuta kama Scrub, chukua mafuta ya nazi yapake kwenye ngozi yako pale tu baada ya kupaka fanya masaji ngozi yako ili ilainike.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv