Ukweli ni kwamba mawazo yetu ndiyo faraja pekee ya maisha. Tukijikubali, kujipenda na kujiwazia mema hatutafadhaishwa na hali yawenzetu kutojali shida zetu, badala yake tutafurahia matatizo yetu kwa tarajio la “yote yanayopita”.

Watu wengi hawafahamu tofauti kati ya UBINAFSI NA BINAFSI kutojua huko ni msingi wa matatizo ya kimaisha kwa wanadamu wengi na ukosefu wa faraja. watu wengi hawajitambui na kujithamini, ndiyo maana wanadhani wamezaliwa ili wateseke hapa duniani.

Ukweli  kwamba kila mmoja wetu angejua kusimama vema kwenye mhimili wa maisha yake tungepunguza kwa kiasi kikubwa mfadhaiko wa mioyo yetu na msongo wa mawazo usiokuwa na sababu.

Ifahamike kwamba mwanadamu wa kwanza aliumbwa BINAFSI Tafsiri ya neno hilo inayopatikana kwenye kamusi ya Kiswahili Sanifu na TUKI toleo la pili ni “kwa nafsi yangu, kwa ajili yangu mwenyewe tu.” 

Popote pale duniani mwanadamu binafsi ndiye mwenye kuishi kwa furaha, ndiye mwenye mafanikio, anayeweza kujifariji mwenyewe kwa umaskini wake, hali yake duni, ugonjwa wake sugu, taabu na shida zake kwa sababu yeye ni mwenyewe tu.

Katika hali ya kawaida, nyuma ya binafsi kuna ubinafsi ambao unaelezwa kwenye kamusi “ni hali ya mtu kujifariji na kujipenda yeye mwenyewe” ambayo kwa mtazamo inaelea hewani na kuwafanya WATU wengi wadhani kuwa maana ya maneno haya ni moja.

Ubinafsi halisi ninaouzungumzia ndiyo huu, ambao unamfanya mwanamke ambaye hajazaa atamani kuzaa kama fulani, amiliki gari, awe na maisha ya juu. Mawazo hayo humsogeza kwenye hali ya kujidharau na hatimaye kufadhaika.

Hii ndiyo sumu ya ubinafsi ambayo inaua, inadhoofisha na kuondoa hali ya uthubutu wa kukabiliana na matatizo yetu kama wanadamu na kutufanya tulilie kusaidiwa au kufarijiwa na wenzetu.
fahamu kwamba ukifadhaishwa na chochote ujue unaumizwa na ubinafsi wako unaokusumbua kutaka uwezo wa mali za mtu mwingine uwe nazo wewe.

Mtu mwenye mawazo ya ubinafsi ikitokea eneo lote analoishi watu wote wana matatizo kama yeye, utashangaa kuona mwanadamu huyo anaishi kwa furaha, si kwa sababu amefanikiwa, bali amekosa aliyemzidi wa kujifananisha naye.

Usijiumize kwa kutaka maisha ya mtu fulani yawe yako kwa ghafla, fanya na kutengeneza yako.

JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz  , twiter@edonetz  , inst@edonetz_blog  na  youtube@edone tv
 
Top