Kama ulikuwa hujui basi jua kwamba Wanawake wajawazito
wanashauriwa kulala kwa upande na sio kulala chali katika miezi mitatu ya
mwisho ya ujauzito ili kupunguza hatari kubwa
ya kujifungua watoto waliofariki tumboni.
Hii ni Kutokana na Utafiti uliofanywa nchini Uingereza Imeelezwa
kuwa wajawazito wengi wanapendelea kulala kwa mgongo (chali) jambo ambalo lina madhara makubwa sana hasa kwa mtoto tumboni hata kuweza kusababisha
kifo.
Utafiti huo
umeonesha takriban mimba 225 nchini Uingereza huharibika na kwamba takriban
maisha ya watoto 130 kila mwaka huokolewa kwa wajawazito ambao hulala kwa
kutumia upande wa kulia ama kushoto.
JIUNGE NASI KWA KUTUFOLLOW
fb@edonetz , twiter@edonetz , inst@edonetz_blog na youtube@edone tv