Aphid(vidukari) ni wadudu wanaoshambulia mazao mbalimbali ,midomo yao imechongoka kama sindano ili kuwasaidia kunyonya virutubisho na maji kwenye mmea na wanaharibu hatua zote za ukuaji wa mmea japo mara nyingi wanapendelea mimea michanga.
Mara nyingi wanakaa chini ya jani au kwenye michipua ya mmea.
Madhara yake
Husababisha jani kujikunja, kukauka ,kupoteza ukijani ,kudumaa ,na mmea unaweza kufa kabisa kulingana na ukosefu wa virutubisho.
Husababisha jani kujikunja, kukauka ,kupoteza ukijani ,kudumaa ,na mmea unaweza kufa kabisa kulingana na ukosefu wa virutubisho.
Pia mmea hushindwa kujitengenezea chakula chake kulingana na kukosekana kwa ukijani na jani kujaa utando ambao hufanya mmea kushindwa kupata hewa.
Hawa wadudu ni hatari sana kwani hueneza ungonjwa wa virusi kwa mmea.
Hatua za kuchukua: kwanza unapowekeza katika kilimo zisipite siku tatu hujakagua (inspect) shamba lako na uonapo wadudu hawa muone mtaalamu wa madawa ya kuua wadudu washambuliao mmea.